Na: Hendrick Msangi
Kuelekea Ufunguzi wa maonyesho ya 6 ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini ambayo yatafunguliwa na Mh Dkt . Dotto Biteko (Mb) , Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati katika viwanja vya EPZ- Bombambili , Geita mjini, Halmashauri ya Wilaya ya Geita chini ya Mkurugenzi wake Ndugu Karia Rajabu, imejipanga vema katika maonyesho hayo.
Katika banda lao, utaweza kuona vitu mbalimbali,ikiwepo uchenguaji wa dhahabu, pamoja na bidhaa mbalimbali kama vile unga Safi wa Muhogo, dagaa, sabuni za maji, batiki na urembo , vyungu vya asili, pamoja na utunzaji wa mazingira ambapo unaweza jipatia michele bora .
Baadhi ya Maafisaa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakiwa Kwenye banda la maonyesho tayari kuwahudumia wananchi
Maonyesho hayo yenye kauli mbiu '' Matumizi ya Teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira " yanatarajiwa kuzinduliwa Leo Septemba 23 na Baadaye kufungwa na Mh Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania septemba 30.
Maonyesho hayo ni fursa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kujitangaza kiuchumi na kuwavutia wadau mbalimbali kuja kutafuta fursa katika Wilaya ya Geita.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa