Mashindano ya Michezo ya Watumishi wa Mamlaka za Serikali za mitaa Tanzania ( Shimisemita) mwaka 2024 yaliyoanza Agosti 24 yamemalizika Septemba 5,2024 katika Jiji la Mwanza.
Akifunga mashindano hayo katika viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Said Mtanda amezipongeza Halmashauri 100 kati ya 184 ambazo zimeshiriki mashindano hayo yaliyokuwa na kila aina ya burudani.
kikosi kutoka Geita Dc baada ya kutangazwa mshindi katika mashindano ya Shimisemita yaliyofanyika jijini Mwanza.
Akikabidhi zawadi kwa washindi katika michezo Mtanda amesema michezo hujenga mahusiano mazuri kwa watumishi na kuzitaka Halmashauri ambazo hazijashiriki mashindano hayo kushiriki ifikapo mwakani. "Michezo ni sehemu kubwa ya maisha yetu kwani huwaweka watumishi pamoja na kujenga mahusiano mazuri" amesema Mhe Mtanda.
Aidha Mhe Mtanda amewapongeza wakurugenzi kwa namna ambavyo wameshiriki katika michezo na Kufanya idadi kufika Halmashauri 100 kulinganisha na mwaka 2023 ambapo zilishiriki Halmashauri 45
"Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inadhamira ya kuinua sekta ya michezo,Sanaa na utamaduni hivyo wakurugenzi endeleeni kuziunga juhudi za mama kwa kuanzisha goli la Mkurugenzi katika Halmashauri zenu". Amesema Mhe Mtanda
kikosi cha mpira wa miguu kikiwa katika mashindano ya Shimisemita.
Pamoja na hayo amelaani baadhi ya Halmashauri kuweka mamluki katika mashindano hayo na kuzitaka kuweka watumishi pindi mashindano hayo yatakapo fanyika tena.
Mashindano hayo yaliyokuwa yamebeba kauli mbiu ya kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa maendeleo ya Taifa endelevu yamemalizika ambapo timu ya mpira wa miguu ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita imeibuka mshindi kwa kuichapa timu ya Halmashauri ya Mji Ifakara magoli mawili kwa moja mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika katika jiji la Tanga mwaka 2025.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita inayo ongozwa na Mkurugenzi Mtendaji ndg Karia Rajab Magaro inawapongeza watumishi wote waliopeperusha bendera ya Halmashauri na kuweza kupata ushindi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa