Katoro-Geita
Ukusanyaji wa mapato ni moja ya agenda ya kudumu katika Vikao vya Timu ya Menejimenti Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Mwaka wa fedha 2024/25 Halmashauri ya Wilaya ya Geita ilivuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 125.19 ambapo Jumla ya Kiasi cha Shilingi Bilioni 10.4 zilikusanywa sawa na ongezeko la Kiasi cha Shilingi Bilioni 2.1 kutoka kwenye Bajeti yake ya shilingi Bilioni 8.3 iliyokasimiwa.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Karia Rajab Magaro amekuwa akiwasisitiza Watendaji wote ndani ya Halmashauri kuendelea kuwa waadilifu katika ukusanyaji wa mapato huku akiwataka kuwa wabunifu kusimamia na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ndani ya Halmashauri.
Kutokana na Usimamizi mzuri wa Mapato ya Ndani, Miradi mbalimbali imetekelezwa kwa mwaka wa fedha 2024/25 kupitia mapato ya ndani ambapo jumla ya kaisi cha Shilingi Bilioni 3.1 kilitengwa kutekeleza miradi zikiwepo Shule, Zahanati, Vituo vya Afya , Nyumba za Watumishi na Ofisi za Kata.
Aidha kupitia mapato ya ndani na fedha za Marejesho, Halmashauri imeweza kutoa Mikopo ya Asilimia 10 kwa Makundi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu ambapo kaisi cha Shilingi Bilioni 1.8 kimetolewa kwa wananchi waliokidhi sifa za kupokea mikopo hiyo.
Ili kuendelea kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha miradi mbalimbali zikiwepo shule, Zahanati, Vituo vya Afya, Miundombinu ya Barabara, Halmashauri imeendelea na mipango ya kutwa maeneo mengi ya uwekezaji ili kuendelea kuinua mapato yake.
Julai 24, 2025 Timu ya Menejimenti Halmashauri ya Wilaya ya Geita ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi CPA Eveline Ntahamba imefanya ziara katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro ili kukagua maeneo ya Uwekezaji.
Timu hiyo imetembelea Eneo lenye ukubwa wa ekari 14 ambapo Halmashauri inatarajia kulitwaa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha magari (Katoro bus stand) Pamoja na Eneo la Soko la Kariakoo Katoro ili kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji katika kuinua mapato ya Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita inaendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo inaleta fedha nyingi kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa