Maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZ Geita mjini yamekuwa fursa muhimu kwa wachimbaji wadogo, wafanyabiashara, wakulima, na wadau wengine wa sekta mbalimbali kupata elimu na kuonyesha bidhaa zao. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita amewakaribisha wananchi na wadau kutembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Geita, ambapo wanapata mafunzo na bidhaa za kipekee.
Mafunzo yanayotolewa katika banda hilo yanalenga kuwaelimisha wachimbaji wadogo kuhusu teknolojia mpya ya kuchenjua madini kutoka kwenye mchanga wenye chembechembe za madini. Hii inalenga kuwasaidia wachimbaji kuongeza tija na ufanisi katika kazi zao za uchimbaji
mashine ya uchenjuaji wa madini ya dhahabu yenye uwezo wa kutenganisha mchanga na madini
Vilevile, maonesho hayo yanatoa fursa kwa wafanyabiashara kuonyesha bidhaa mbalimbali kama dagaa kutoka Ziwa Victoria, mafuta ya kupikia, sabuni za maliwato, mbegu za mahindi, na mvinyo bora kutoka Igate. Pia, mafunzo ya kilimo cha miti ya mbao, matunda, na ufugaji wa bata mzinga yanatolewa kwa lengo la kuwawezesha wakulima kuboresha uzalishaji na kuongeza kipato.
Dagaa kutoka ziwa Viktoria maarufu kama dagaa wa Mwanza
Kilimo cha mihogo
Ufugaji wa bata mzinga
Mvinyo unaotengenezwa na kikundi cha kina mama kutoka Igate.
Mafuta safi ya kupikia
Sabuni yenye maliwato mazuri
Mbegu bora za Mahindi
Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Bi. Mathalena Mgina, ameeleza kuwa mafunzo na bidhaa zinazotolewa katika banda hilo ni za asili, na wananchi wengi wamejitokeza kwa wingi kujifunza na kupata elimu hiyo.
Maonesho hayo yalianza Oktoba 1 na yanatarajiwa kumalizika Oktoba 12, 2024, huku yakiwa na kauli mbiu inayosisitiza "Matumizi ya Teknolojia na Nishati Safi Katika Sekta ya Madini kwa Maendeleo Endelevu."
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa