Spika Mstaafu wa Bunge na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Anne Makinda, amesema ni muhimu kuimarisha elimu ya umuhimu wa takwimu ili kuhakikisha matumizi sahihi kwa wananchi na kusaidia ujenzi wa jamii yenye uelewa wa masuala ya takwimu kwa maendeleo endelevu.
Spika Mstaafu wa Bunge na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Anne Makinda, Akitoa hotuba mbele ya maafisa habari wa Mikoa na Halmashauri ya kanda ya ziwa katika mafunzo.
Makinda aliyasema hayo alipofungua mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika Machi 17 na 18, 2025, katika Mkoa wa Simiyu. Mafunzo hayo, yaliyoratibiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), yalilenga kuimarisha vitengo vya mawasiliano katika ngazi ya halmashauri na mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Maafisa mawasiliano kutoka Halmashauri na Mikoa ya kanda ya Ziwa wakiwa katika mafunzo.
Katika hotuba yake, Makinda aliwataka washiriki kuhakikisha elimu ya takwimu inawafikia wananchi kwa ngazi zote ili kurahisisha upatikanaji na matumizi yake kwa maendeleo ya jamii. Aidha, alisisitiza umuhimu wa NBS kushirikiana kwa karibu na ofisi za mawasiliano katika ngazi mbalimbali ili kuhakikisha taarifa za takwimu zinaeleweka kwa umma na zinatumika ipasavyo.
Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa hatua ya tatu ya Sensa ya Watu na Makazi, inayohusisha usambazaji wa matokeo na matumizi yake kwa maendeleo ya taifa.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa