Katoro-Geita
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi amesema Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelinda heshima ya kiongozi aliyemtangulia kwa kuendeleza miradi mikubwa afrika Mashariki.
Mamia ya wananchi wakiwa katika viwanja vya CCM-Katoro wakifuatilia Mkutano wa Hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM), Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi
Akizungumza na wananchi kata ya Katoro halmashauri ya wilaya ya Geita wakati wa ziara yake Agosti 12, 2024, Balozi Dkt Nchimbi ameitaja miradi mikubwa Mhe Dkt Samia ameiendeleza ni pamoja na mradi wa treni ya umeme kutokea Dar es Salaam kwenda Mwanza ambayo Hayati Magufuli alianza kuijenga na hadi kifo chake mradi huo ulikuwa umefika KM 722 na kusema Mhe Dkt Samia katika awamu yake ameweza kujenga km 1506 na kwa upande wa mradi wa bwawa la umeme ambao ulikuwa umefika asilimia 36 ambazo ziliachwa na mtangulizi wake na kwa sasa mradi huo umefika asilimia 98.4. “Amelinda heshima ya kiongozi aliyemtangulia” amesema Balozi Dkt Nchimbi.
Mhe Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela akizungumza katika Mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Uliofanyika Kata ya Katoro ambapo, Balozi Dkt Nchimbi amepongeza uongozi mzuri wa Mkuu huyo wa Mkoa katika kusimamia shughuli za kiserikali ndani ya Mkoa wa Geita.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Busanda wilaya ya Geita Mhandisi Tumaini Magesa amemuomba katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi, kuendelea kushughulikia suala la hitaji la kuwa na Halmashauri kwa wananchi wa jimbo la Busanda kwakuwa kumekuwa na idadi kubwa ya wananchi
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM) Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi amehutubia mamia ya wananachi katika viwanja vya CCM-Katoro ambapo amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amelinda heshima ya kiongozi aliyemtangulia kwa kuendeleza miradi mikubwa ikiwepo ya ujenzi wa Reli ya kisasa
Naye Naibu Waziri wa mambo ya ndani Daniel Bassil Sillo amesema kuwa serikali imeanza mchakato wa kuupandisha hadhi ya mji mdogo wa katoro kuwa wilaya ya Kipolisi ili kuendelea kuboresha huduma za usalama katika mji huo kutokana na kuwa naongezeko kubwa la watu. Sillo amesema amepokea changamoto hiyo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhandisi Magesa juu ya ombi la mji huo kuwa Halmashauri.
Pamoja na hayo ziara ya Mhe Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi imelenga kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia majibu ambapo jumla kero 108 kutoka kwa wananchi 61 zilipokelewa na kutoa ufumbuzi wa kero hizo, huku baadhi zikikabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela kuzishughulikia.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa