Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Afya na Mbunge wa Jimbo la Busanda, Mh. Dkt. Jafari Rajabu, leo Disemba 18, amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita pamoja na kukutana na watumishi, huku akiwasisitiza juu ya suala la ufanyaji kazi kwa weledi na kuzingatia miiko ya taaluma zao.
Mhe. Dkt. Jafari amesema kuwa lengo la serikali ni kuleta huduma bora kwa wananchi na hivyo Watumishi wa Umma wanapaswa kuwa mstari wa mbele kwenye kutekeleza kwa vitendo maono hayo ili kuacha alama kwenye maeneo yao ya kazi.
"Watumishi wa umma tuna wajibu wa kuwahudumia raia wote kwa usawa. Hivyo tunapaswa kutambua kuwa tunatakiwa kufanya kazi kwa weledi pasi na kuendekeza uzembe na ubadhirifu kwenye ofisi za umma." Amesema Dkt. Jafari.
Mhe. Waziri pia ametoa rai kwa Halmashauri kuongeza ubunifu kwenye ukusanyaji wa mapato haswa kwenye sekta za Uchimbaji, Uvuvi, Misitu, Maliasili na Utalii, pamoja na kuibua miradi ya kimkakati na endelevu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Geita, Ndg. Hashim Komba ameipongeza serikali kwa kuongeza bajeti kwende eneo la miundombinu ya barabara kupitia TARURA, pamoja na kuwataka wakuu wa idara kuyafanyia kazi maagizo ya Naibu Wazir, ili Halmashauri ya Wilaya ya Geita iwe mfano kwa Halmashauri nyingine.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa