Nzera-Geita.
Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita umeendelea kwa siku ya pili leo Februari 4,2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri uliopo Nzera.
Akizungumza katika Mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Karia Rajab Magaro amesema Halmashauri imefanikiwa Kukusanya Shilingi Bilioni 6.3 ya mapato ya ndani sawa na asilimia 45.42 ya mapato yaliyotarajiwa kukusanywa kwa mwaka.
Kufuatia mafanikio hayo Magaro amewashukuru Waheshimiwa Madiwani kwa namna wanavyosimamia jukumu la ukusanyaji wa mapato.
" Tunawashukuru sana Wah Madiwani kwa kusimamia jukumu la ukusanyaji wa mapato ambapo mmekuwa bega kwa bega na Menejimenti katika Kushauri na kusisitiza ukusanyaji wa mapato katika vikao mbalimbali" Amesema ndg Magaro.
Vilevile Ndg Magaro amesema Halmashauri imepanga kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 20.9 kutokana na mapato ya ndani, wahisani na Serikali Kuu.
" Jumla ya Shilingi Bilioni 6.7 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu na wadau" Amesema Ndg Magaro.
Pamoja na hayo, Ndg Magaro amesema Halmashauri kupitia mapato ya ndani imetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 4.7 katika kutekeleza miradi ya maendeleo ili wananchi wanufaike.
" Nitoe rai kwa Waheshimiwa Madiwani kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ili kupata thamani ya Fedha (Value of Money) iliyotolewa.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji ametumia Mkutano huo wa Baraza la Madiwani kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa namna ambavyo wamekuwa chachu kwa kushiriki kufanya utuatiliaji katika kuhakikisha Halmashauri inapata fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.
Akihitimisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za Maendeleo kwa ngazi ya Halmashauri kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2025, Mkurugenzi Mtendaji ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo ongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuiewezesha Halmashauri kupokea fedha nyingi za miradi ya maendeleo ambapo imeenda kupunguza adha ambazo wananchi walikuwa wakizipata.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa