Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Karia Rajab Magaro amewaagiza wakuu wa shule za sekondari kuchukua hatua kwa walimu wanaoshindwa kuwajibika kutekeleza majukumu yao.
Agizo hilo amelitoa wakati wa kikao cha Afisa Elimu sekondari na Wakuu wa shule kilichofanyika katika shule ya sekondari Geita chenye lengo la wakuu wa shule kujadili mikakati,malengo, na mipango ya kuinua kiwango cha ufaulu kwenye Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Karia amewataka wakuu wa shule kuchukua hatua kwa walimu ambao hawatimizi majukumu yao ikiwa ni pamoja na wale wanaokunywa pombe wakati wa kazi.
Aidha amewataka wakuu wa shule kwenda kusimamia kikamilifu miradi inayojengwa katika shule zao ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Kaimu afisa elimu sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Geita Richard Makoye amewasisitiza wakuu wa shule pamoja na walimu wao kwenda kuwajibika katika majukumu yao.
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni mkuu wa shule ya sekondari ya Katoro George Hezron amewataka walimu wote kuwajibika kwa kuwa Mkurugenzi ameahidi kutoka zawadi kwa walimu watakaofanya vizuri katika masomo wanayofundisha.
Wakuu wa shule 74 wameshiriki kikao hicho huku 71 wakiwa ni wa shule za Serikali na 3 wa shule za binafsi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa