Na: Hendrick Msangi NZERA.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndugu Karia Rajabu Magaro, amefanya ziara kwenye jengo jipya la Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Mhandisi Shilingo akimuonyesha ramani ya Jengo la Halmashauri kwa Mkurugenzi ndugu Karia Rajabu Magaro alipotembelea jengo hilo kukagua hatua za ujenzi wake.
Katika Ziara yake yenye lengo la kukagua hatua za ujenzi wa Jengo hilo.
Magaro aliambatana na Wakuu wa Idara mbalimbali za Halmashauri ili waweze kuona kazi inavyoendelea na pia kushauri hatua za kuchukua kuelekea kukamilika kwa jengo hilo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndugu Karia Rajabu Magaro akizungumza na wakuu wa Idara mbalimbali Kwenye Halmashauri hiyo alipotembelea kukagua ujenzi wa Jengo hilo ambalo watumishi wa Halmashauri watahamia Mwezi Octoba.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi Magaro alimtaka Mhandisi Shilingo ambaye ni Kaimu Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuhakikisha anafuatilia mafundi kuwepo site muda wote ili kukimbizana na kazi iliyobaki, pamoja na kuhakikisha vifaa vyote yakiwemo materials ambayo hayajatumika yanahifadhiwa sehemu salama pamoja na kuwa Documented kutunza kumbukumbu.
Aidha alimtaka Mhandisi Shilingo kufanya kazi kwa kasi huku ramani ya jengo hilo ikizingatiwa.
‘’ Unatakiwa uwe Site Engeneer badala ya kukaa ofisini ili kuja kujionea kazi ambazo mafundi wanazifanya na kutoa ushauri wa kitaalam’’ alisema Magaro.
Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo ilipendekeza kuwe na kamati maalum kwa ajili ya kuratibu kazi zote zilizobaki ili kufikia lengo la kuhamia katika jengo hilo.
‘’Kuwe na kamati yenye mpango mkakati na ije na mrejesho wa hatua zilizochukuliwa kukamilisha kazi hii ili tunaposema tunaingia mwezi wa kumi tufikie hilo lengo na iwapo kuna changamoto basi nielezwe’’; alisema Magaro kwa watumishi hao.
Ujenzi wa Jengo hilo ulio anza tarehe 22 mwezi Februari mwaka 2022 unakaribia kukamilika mapema mwezi ujao , na watumishi kuingia rasmi ifikapo Octoba 15, mwaka huu.
Gharama za Ujenzi zilizotumika mpaka sasa ni kiasi cha shilingi Bilioni mbili na laki saba ambazo zimejumuisha ujenzi wa jengo la utawala, uzio, majengo ya kibenki, kibanda cha mlinzi na kibanda cha nishati ya umemeKwa mujibu wa Mhandisi Shilingo , Ujenzi wa Jengo hilo umekamilika kwa Asilimia 95 mpaka sasa.
Ujenzi huo ni sehemu ya miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo Serikali kuu inayo ongozwa na Mh Dkt Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelekeza fedha nyingi kwenye miradi ili kuwaletea wanachi huduma bora na maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa