• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

DC SHIMO MGENI RASMI UZINDUZI WA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI GEITA DC

Posted on: November 24th, 2022

Na. Michael Kashinde

Wakati ambapo Mkoa wa Geita unatarajia kuadhimisha Siku 16 za kupinga ukatili, kwa kuongozwa na kaulimbiu isemayo ‘’Kila Uhai una thamani, Tokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto’’ Halmashauri ya Wilaya ya Geita imepanga kufanya uzinduzi wa maadhimisho hayo Novemba 29, katika Kata ya Katoro, ambapo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Wilson Samwel Shimo.

Siku 16 za maadhimisho hayo zinaanza Novemba 25, hadi Disemba 10, 2022 ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kupinga ukatili wanatarajia kutumia siku hizo kutekeleza shughuli mbalimbali kama vile kuandaa mijadala na wanafunzi mashuleni, kuelimisha jamii kupitia vipindi vya radio na kutoa elimu ya Saikolojia kwa wahanga wa masuala ya akili katika maeneo mbalimbali.

Shughuli nyingine zitakazotekelezwa katika maadhimisho hayo ni pamoja na huduma za kisheria zitakazofanyika katika wiki ya Msaada wa kisheria, huku Shirika la Voluntary Service Overseas (V.S.O) likipanga kufanya mdahalo na wanaume tu (Men’s Talk) Novemba 25 katika Kata ya Nyarugusu, ambapo wanaume wamelengwa katika mdahalo huo kwa kuwa wanaume wanaonekana kuwa wahusika wa ukatili katika jamii.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bw. Alex Herman Novemba 24, 2022 akiwa na wadau hao wa kupinga ukatili katika kikao cha kujadili utekelezaji wa shughuli mbalimbali zitakazofanyika katika siku hizo za maadhimisho hayo ametoa wito kwa wadau hao kusaidia pia ukatili dhidi ya watoto wa kiume.

Bw. Alex amesema kuwa ni vyema jamii ikawa karibu na kufuatilia nyendo za watoto wa kiume pia kuanzia mashuleni kwa kuhamasisha uangalizi wa karibu ili kuwaepusha watoto hao kufanyiwa ukatili ambao unachangiwa na mmomonyoko wa maadili, hali inayopelekea pia kuongezeka kwa matendo ya mapenzi ya jinsia moja suala ambalo ni mmomonyoko mkubwa wa maadili.

Maadhimisho hayo ya kupinga ukatili kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita yanatarajia kuwashirikisha wadau na mashirika mbalimbali wakiwemo Plan International, Nelico, Kivulini, V.S.O, Sedit, Patwao, Rafiki SDO, Gelac na Bright Light.

Aidha wadau na mashirika mengine ni pamoja na Gelao, Marafiki wa Elimu,  Mwanasheria Geita DC, Polisi dawati la Jinsia, TWCC Jinsia na The Golden Line (Walter).

Tangazo

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA IMETOA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI May 24, 2022
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA INAKUTANGAZIA UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA MTAKUJA KATIKA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA KATORO June 15, 2022
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA IMETOA TANGAZO LA KUWAITA KWENYE USAILI WATENDAJI WA VIJIJI NA MADEREVA June 27, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI GEITA DC July 08, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI GEITA DC LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 87.2 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

    January 24, 2023
  • GEITA DC YAWEKA KAMBI KATIKA KATA YA NYARUGUSU KUTOA MSAADA WA KISHERIA

    December 14, 2022
  • DC SHIMO ATAJA UMOJA NA MSHIKAMANO KUWA NGUZO KUU YA MAENDELEO TUNAPOSHEREHEKEA MIAKA 61 YA UHURU

    December 07, 2022
  • RC SHIGELA ATOA RAI KWA JAMII KUITUMIA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KUTAFAKARI NAMNA YA KUPAMBANA NAO

    December 01, 2022
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa