Na: Hendrick Msangi
OPERESHENI ya Kukagua Miradi ya Maendeleo na Kusikiliza Kero za Wananchi Halmashauri ya Wilaya ya Geita imeendelea May 17, 2024 kwa kata ya Bujula katika Vijiji vinne vya kata hiyo ambavyo ni Mduhani, Ngula, Bujula na Nyamiboga.
Ambapo amekagua Miradi ya Maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya Bujula na madarasa 2 shule ya Msingi Ngula, ujenzi wa madarasa manne Mduhani, ujenzi wa nyumba ya mtumishi nyamiboga na mradi wa zahanati na nyumba ya mtumishi.
Katika Ziara hiyo, Mhe Komba ameonyesha kutokutupendezwa na ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya Msingi Nyamiboga yenye thamani ya Shilingi milioni 21 ambazo hazina thamani ya ujenzi wa nyumba hiyo na kuunda Kamati ndogo ya uchunguzi kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupanda na rushwa (TAKUKURU) wilayani Geita kuchunguza Mradi wa Ujenzi wa nyumba hiyo ya Mwalimu iliyojengwa kwa kiasi cha shilingi Milioni 21 baada ya kubaini fedha zilizotumika kutokwendana na thamani ya Mradi huo.
" Tumeliangalia jengo pamoja na Wahandisi thamani yake ni shilingi Milioni 9.2 lakini tuna ambiwa limetumia milioni 21 (CSR). Mchwa wa namna hii wanaotafuna fedha za miradi wanahitaji oili. Tunataka hela za umma zifanye kazi iliyokusudiwa."amesema DC Komba
Nyumba ya Mwalimu shule ya Msingi nyamiboga yenye thamani ya shilingi milioni 21.
Aidha amekemeaa na kutoa onyo kali tabia ya wananchi kuwapa watoto wa kike mimba na kukatishwa ndoto zao na wazazi kuficha taarifa ili kesi zisiende mahakamani kwa makubaliano ya kupeana Mahari
" Walindeni watoto wa Kike, na atakayebainika kukatisha ndoto za Wanafunzi wa kike hatua kali zitachukuliwa. Wazazi tuwalinde watoto kwani urithi pekee ni elimu" amesema DC Komba.
Baadhi ya Wananchi wa kata ya Bujula wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba kwenye Mkutano wa hadhara.
Akihitimisha Ziara hiyo kwa kata ya Bujula, Mhe Komba amewataka Wananchi kuendelea kuwa na imani na Serikali inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kumuunga mkono juhudi zake za kuwaletea Maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba alievaa shati nyeupe aliyeshikilia kalamu akiongozana na Diwani wa kata ya Bujula wa kwanza kulia Bi Amina Swedy aliye weka mtandio begani wakielekea kwenye eneo la mradi.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bujula Mhe Amina Swed amemshukuru Mhe Mkuu wa Wilaya kwa Ziara hiyo na kumuomba kuendelea kuchochea kasi ya Maendeleo ili zahanati zikamilike kuhudumia Wananchi wa kata hiyo ambao wanaenda kutibiwa kata ya Bukoli kutokana na Kata hiyo kukosa Zahanati iliyo kamilika.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba akiwa amekaa kwenye msingi katika Moja ya mradi katika kata ya Bujula.
Pichani wa katikati aliyeshikilia kalamu na WA kwanza kulia aliye kaa ni Diwani wa kata ya Bujula Amina swedi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa