Butundwe-Geita
MKUU wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa MPOX baada ya Waziri wa Afya Mhe Jenista Mhagama (MB) kutangaza kuwepo kwa wagonjwa wawili wa ugonjwa huo.
Tahadhari hiyo imetolewa leo Machi 11,2025 wakati wa Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo na Kusikiliza Kero za Wananchi Katika Tarafa ya Butundwe Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba akizungumza na wananchi katika Mkutano wa Hadhara Tarafa ya Butundwe
Pamoja na kutoa Tahadhari hiyo Mhe Komba amesikiliza na kutatua kero mbalimbali ziliwepo migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, uwepo wa wanyamapori hatarishi , mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Vilevile katika Ziara hiyo Mhe Komba ametembelea na kukagua hatua za ujenzi wa miradi ya elimu na afya ambapo ametoa maelekezo kwa Uongozi wa Halmashauri kukamilisha miradi hiyo ili iwanufaishe wananchi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt Modest Buchard akizungumza na Wananchi katika Ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba iliyofanyika Tarafa ya Butundwe
Katika Ziara hiyo Mhe Mkuu wa Wilaya aliambatana na Katibu Tawala Wilaya ya Geita Bi Lucy Beda, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dkt Modest Burchad pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa MPOX baada ya Waziri wa Afya Mhe Jenista Mhagama (MB) kutangaza kuwepo kwa wagonjwa wawili wa ugonjwa huo.
Tahadhari hiyo imetolewa leo Machi 11,2025 wakati wa Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo na Kusikiliza Kero za Wananchi Katika Tarafa ya Butundwe Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Pamoja na kutoa Tahadhari hiyo Mhe Komba amesikiliza na kutatua kero mbalimbali ziliwepo migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, uwepo wa wanyamapori hatarishi , mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Vilevile katika Ziara hiyo Mhe Komba ametembelea na kukagua hatua za ujenzi wa miradi ya elimu na afya ambapo ametoa maelekezo kwa Uongozi wa Halmashauri kukamilisha miradi hiyo ili iwanufaishe wananchi.
Katika Ziara hiyo Mhe Mkuu wa Wilaya aliambatana na Katibu Tawala Wilaya ya Geita Bi Lucy Beda, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dkt Modest Burchad pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Matukio mbalimbali katika Picha wakati wa Ziara ya Mhe Mkuu wa Wilaya ya Geita Hashim Komba alipofanya Ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo na Kusikiliza Kero za Wananchi Tarafa ya Butundwe Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa