Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba Julai 29, 2024 amefanya Ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kata ya Kakubilo na Kusikiliza Kero za Wananchi.
Awali akimkaribisha katika kata hiyo Diwani wa kata ya Kakubilo Mhe Kesi Igayo Nyanda ameomba uongozi wa Halmashauri kuwapa kipaumbele mafundi wazawa katika Kutekeleza miradi ya maendeleo katika kata hiyo badala ya kuwa na mafundi wanaotoka nje ya kata hiyo.
Akiwa Katika kata ya Kakubilo Mhe Komba ametembelea Miradi ya Maendeleo katika Kijiji cha Nyabalasana ambapo amekagua ujenzi wa jengo la utawala katika shule ya Sekondari Nyabalasana unaotekelezwa na mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) kwa gharama za Shilingi milioni 100,485,779.88 na kiasi cha shilingi 10,010,000 zikiwa nguvu za wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba amekagua mradi wa jengo la utawala katika shule ya Sekondari Nyabalasana unaotekelezwa na mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) kwa gharama za Shilingi milioni 100,485,779.88 na kiasi cha shilingi 10,010,000 zikiwa nguvu za wananchi.
Kwa upande mwingine Mhe Komba amewataka wahandisi kusimamia vema Miradi ili iwe na kiwango sawa na fedha inayotolewa na Serikali." Kila mtumishi akae kwenye nafasi yake kazi zifanyike vizuri" amesisitiza Mhe Komba.
Mhe Komba akikagua mradi wa zahanati kijiji cha Kabayole kata ya Kakubilo ulionzishwa kwa nguvu za wananchi. Uongozi wa Halmashauri umesema kupitia mapitio ya bajeti, mapato ya ndani na CSR Utawezesha kukamilisha zahanati katika kata hiyo ili kuendelea kusogeza huduma kwa wananchi
Katika kuendelea na Ziara hiyo, Mh Komba ametembelea ujenzi wa Kituo cha Afya Kakubilo ambacho Diwani wa kata hiyo Mhe Kesi Igayo Nyanda ameomba kituo hicho kuanza kutumika ili Wananchi waanze kupata huduma za kiafya ili kupunguza umbali mrefu wa kufuata huduma katika kata za jirani.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba akizungumza na mamia ya wananchi wa Kata ya Kakubilo alipofanya mkutano wa hadhara ambapo amewataka kuacha matendo ya kikatili kwa kukatiza uhai wa watu wenye Ulemavu wa ngozi na kuwataka wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu.
Miradi Mingine ambayo Mhe Komba ametembelea akiwa na wakuu wa Taasisi,Idara na vitengo ni ujenzi wa zahanati ya kabayole ambao umeanza kwa nguvu za wananchi ambao umesha ezekwa, Zahanati ya Kijiji cha Luhara ambayo ipo hatua ya boma.
Mbali na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo, Mhe Komba aliweza sikiliza Kero za wananchi na kuzitolea majibu zikiwepo kero za wanufaika wa TASAF ambapo amesema Serikali imetoa maagizo kwa kaya masikini kuwezeshwa pamoja na kuwaletea wananchi Miradi ya Maendeleo katika maeneo yao.
Mradi wa Kituo cha Afya Kakubilo ambao unatarajiwa kuanza kutumika ifikapo Mwezi Septemba 2024. Mradi huo utasaidia kupunguza umbali wa wananchi kufuata huduma maeneo mengine.
Aidha ameitaka Idara ya Maendeleo ya jamii kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya mikopo inayotolewa na Serikali ambayo haina riba ili wananchi waweze kukopa na kuepukana na mikopo almaarufu kama kausha damu.
Akihitimisha ziara katika kata ya Kakubilo Mhe Komba amewasihi Wananchi kuacha matendo ya kikatili kwa kukatiza uhai wa watu wenye Ulemavu wa ngozi na kuwataka wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu. "Kujichukulia sheria mkononi ni jambo ambalo halikubaliki hivyo toeni taarifa kwa Wote wanaojihusisha na tabia za kikatili." amesisitiza Mhe Komba.
Mamia ya wananchi wa kata ya Kakubilo wakifuatilia mkutano wa Hadhara wa Mkuu wa Wilaya ambapo walisikilizwa kero zao na kupatiwa majibu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa