Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kuendelea kuwasimamia wakandarasi ili waweze kukamilisha miradi kwa wakati kabla ya kutembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru, 2025.
Akizungumza hapo Jana, Mei 5, wakati akikagua mradi wa Shule ya Sekondari ya Amali, Kata ya Nzera kwenye ziara maalumu ya ukaguzi wa njia iliyopendekezwa kupitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru, Mhe. Komba amesema ameridhishwa na kasi inayoendelea kwenye hatua ya umaliziaji wa mradi huo, huku akiiagiza Halmashauri kuhakikisha inatoa fedha kwa wakati ili kazi zilizosalia ziweze kufanyia kwa haraka, kwa kuzingatia ubora.
Mkuu wa Wilaya pia aliiagiza Halmashauri kuhakikisha kwenye mradi huo, huduma zote za msingi kama vile Maji na Umeme, zinapatiwa ufumbuzi huku nyaraka muhimu za Hati ya eneo hilo zinapatikana kutoka ofisi ya ardhi pamoja na madeni ya wahusika yanalipwa kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa