• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

DC KOMBA AAGIZA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI KUWA NA DAWATI LA MALALAMIKO LINALOTEMBEA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI-GEITA DC

Posted on: March 23rd, 2024

Na:Hendrick Msangi

WANANCHI wa Kata ya Nkome Halmashauri ya Wilaya ya Geita wamesisitizwa kujenga utamadini wa kuchangia pato la Taifa ili kuendelea kuijenga halmashauri kwa kuendelea kulipa tozo zinazotakiwa kwa kila biashara wanayoifanya pamoja na kujenga utamaduni wa kuendelea kuisimamia miradi ya maendeleo katika maeneo yao  ili kumuunga mkono Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yameelezwa Machi 22, 2024 wakati Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba alipofanya ziara kwenye Kata ya Nkome kusikiliza kero na changamoto za wananchi wa kata hiyo ambayo wananchi wengi wa kata hiyo hujishughulisha na shughuli za uvuvi.

Wananchi wa Kata ya Nkome wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba kwenye mkutano wa hadhara ambapo kero mbalimbali za wananchi hao zilipatiwa majibu. Wananchi hao walisisitizwa kutokukaa na kero muda mrefu kwani serikali ya awamu ya sita ipo kuwasikiliza na kutatua kero na changamoto zinazowakabili.

Wananchi walipata fursa ya kueleza kero zao kwa Mkuu wa Wilaya ambapo baadhi ya kero walizo lalamika mbele ya Mkuu wa Wilaya ni pamoja na  wingi wa michango mashuleni ikiwa ni michango ya mitihani na chakula huku wanafunzi wasiochangia kurudishwa nyumbani,  wananchi kuuziwa nyumba zao na madalali pasipo amri ya mahakama, tozo za dagaa na samaki kwa wavuvi, magari ya abiria kutokufika kituo cha mabasi, mikopo ya vikundi vya ujasiriamali pamoja na kaya zinazonufaika na mfuko wa Tasaf wahusika wakidai kutokupata fedha hizo.

Akijibu kero hizo katika Mkutano mkubwa wa hadhara, Mhe Komba alikemea tabia ya uchangishaji wa michango mashuleni ambayo haijapata kibali kutoka serikalini.”Nimarufuku kwa shule zetu kuwa na michango ambayo ni holela,na ambayo haijapata kibali cha serikali kutoka ofisiya Mkuu wa Wilaya.” Alisema Mkuu wa Wilaya.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba akizungumza na wananchi wa Kata ya Nkome alipofanya ziara kwenye kata hiyo kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua ikiwa ni agizo la Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wananchi wasikilizwe kero zao na kuzitatua.

Kuhusu swala la Lishe, aliwataka wazazi na walezi kutambua kuwa ni wajibu wao kuhakikisha watoto wanapata lishe wawapo shuleni kwa kufanya makubaliano kwani ni jambo la lazima shuleni. Mh Komba alikemea tabia ya kuwafukuza au kuwaadhibu watoto shuleni kwa sababu wazazi wao hawajatoa hela za chakula bali kuwataka walimu kuwafuatilia wazazi na walezi wao ili watoto wapate chakula kwa kipindi wawapo shuleni.

Akizungumzia swala la wananchi kuuziwa nyumba zao na madalali, Mhe Komba alikemea tabia hiyo na kusema kumekuwa na tabia za  madalali wasio kuwa na amri ya mahakama kupiga mnada nyumba za   wananchi.

Kilio cha wananchi kutoka kaya masikini ambao wamekuwa wakinufaika na fedha za mfuko wa TASAF kilimfikia Mkuu wa Wilaya ambapo alitoa maelekezo kwa waratibu wa mfuko huo wa kunusuru kaya masikini kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kutambua wenye sifa na wasio na sifa za kupewa fedha hizo ili kuepuka malalamiko kwa wananchi kwani malalamiko mengine ni kukosa elimu kunakopelekea wanachi hao kulalamika.

Akitolea majibu kero ya mikopo kwa wajasiriamali, Mkuu wa Wilaya aliiagiza ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kutoa maelekezo kwa watendaji wa kata na vijiji kufanya mikutano ya wananchi ili kutoa elimu juu  ya fedha zinazoletwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wananchi, pamoja na kuwasaidia wananchi kutengeneza vikundi  ambavyo vitaorodheshwa  ili kuweka uwazi wa fedha iliyotolewa na vikundi vilivyo nufaika na fedha hizo kufahamika na wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba akiwasikiliza wananchi katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika kata ya Nkome. Pamoja na kusikiliza kero zao, Dc Komba aliwataka wananchi hao kujenga  utamadini wa kuchangia pato la Taifa ili kuendelea kuijenga halmashauri kwa kuendelea kulipa tozo zinazotakiwa katika biashara zao

Ili kuendelea kutatua kero za wananchi , Mhe Mkuu wa Wilaya alitoa maagizo kwa watendaji wa kata kuwa na dawati la malalamiko  linalotembea kuwasikiliza wananchi  ili kusogeza huduma jirani na wananchi kwani zipo kero ambazo zinaweza kutatuliwa katika ngazi ya kijiji au kata. “Watumishi nendeni mkawasikilize wananchi katika maeneo yao ili kushughulikia kero zao, tumeajiriwa ili kuwatumikia wananchi” alisema Mhe Mkuu wa Wilaya.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba akipokea taarifa ya mradi wa kituo cha mabasi kata ya Nkome kilichojengwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri kiasi cha Tshs. 79,000,000 Ambapo kiasi cha Tsh. 29,900,000 kilihamishwa TARURA kwa ajili ya ujenzi wa Barabara km 1 kutoka Nkome centre hadi stendi na kusawazisha eneo la stendi na kiasi kilichobaki Tsh. 49,100,000 kilitumika kujenga miundombinu ya stendi ikiwa ni ujenzi wa choo matundu 6  na vibanda 2.

Mwisho Mkuu wa Wilaya aliwashukuru wananchi wa Kata ya Nkome kwa kujitokeza kwa wingi kwenye Mkutano huo na kuwataka wasikae na malalamiko muda mrefu huku akiwasisitiza kushikamana na viongozi wao  ikiwa ni pamoja na kuwa kuwa na utamaduni wa kuchangia kwenye mapato ya Halmashauri ili kuiwezesha halmashauri kufanya shughuli za maendeleo.     

Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC KOMBA ARIDHISHWA NA UTEKEKEZAJI WA MIRADI KUELEKEA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025.

    May 06, 2025
  • MEI MOSI YALETA FARAJA KWA MAAFISA TARAFA GEITA.

    May 02, 2025
  • RC SHIGELA AIBUA MATUMAINI MAPYA KWA WATUMISHI MKOANI GEITA.

    May 02, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI GEITA DC LAMPONGEZA MKURUGENZI MTENDAJI KWA KUPATA HATI SAFI

    April 30, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa