Kampuni ya uchimbaji madini ya Buckreef imesaini mkataba wa TZS milioni 600 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya afya na elimu kupitia mpango wake wa CSR mkoani Geita. Uwekezaji huu unalenga kuboresha huduma muhimu kwa wananchi wanaoishi karibu na mgodi.
Hafla ya utiaji saini ilishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Geita na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, ambao wamesisitiza usimamizi makini wa miradi ili iwe na manufaa ya moja kwa moja kwa jamii.
Viongozi wa Kata mbalimbali pia wameipongeza Buckreef kwa kuendelea kuwa mshirika wa maendeleo, wakieleza kuwa ushirikiano kati ya mgodi na jamii umeendelea kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya kijamii katika maeneo yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa