NZERA-GEITA
BENKI ya CRDB Tawi la Geita imetoa Kiasi cha Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa Wawili katika Shule ya Msingi Fulwe iliyopo Kata ya Nzera .
Hayo yamejiri leo Machi 7,2025 ambao Wataalam kutoka Benki ya CRDB Tawi la Geita walipoitembelea Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na kukaribishwa katika Kikao cha Kawaida cha Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango.
Akizungumza katika Kikao cha kawaida cha Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri-Nzara Machi 07.2025, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Charles Kazungu ameishukuru Benki hiyo kwa kuongeza huduma za kibenki katika Halmashauri.
"Tunashukuru Benki ya CRDB Tawi la Geita kwa kusogeza huduma ndani ya Halmashauri lakini pia Tuwaombe muweze kuona namna ya kuanza kuyatumia majengo ya Kibenki ambayo yamengwa na Halmashauri ili yaanze kutumika." Amesema Mhe Kazungu.
Kwa upande wake Meneja wa tawi wa Benki hiyo ndugu Erick Mgala amesema Benki hiyo imetoa kiasi cha Shilingi Milioni 50 kama sehemu ya kurejesha huduma kwa jamii.
Aidha Mgala amesema Halmashauri ya Wilaya ya Geita imekuwa ikishirikiana na Benki ya CRDB katika mambo mengi na kuahidi kuendeleza ushirikiano.
Vilevile Meneja huyo amesema kufuatia kilio cha wananchi wa kata ya Nzera kukosa kwa karibu huduma za Kibenki , CRDB imesikia kilio Chao na imepanga kuleta gari ambalo ni benki inayotembea kwa ajili ya kutoa huduma za kibenki katika maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri.
Naye Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Fulwe Mwl Mathias Bulabo ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuona umuhimu wa kuongeza madarasa Katika shule hiyo.
Shule ya Msingi Fulwe ilianzishwa Januari 1956 na kwa mwaka wa masomo 2025 ina jumla ya Wanafunzi 598 Wavulana wakiwa 276 na Wasichana wakiwa 322 na Jumla ya Vyumba vya madarasa 14 huku ikiwa na Jumla ya Walimu 13.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita ina wakaribisha wadau mbalimbali wa maendeleo na itaendelea kushirikiana na wadau wote katika kuendelea kutekeleza shughuli za maendeleo ndani ya Halmashauri yenye Jumla ya Kata 37.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa