Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Januari 25, 2022 limejadili na kupitisha Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 inayopendekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi bilioni 81, milioni 151,laki 7, 22 elfu na 890. (Tshs.81,151,722,890)
Akiwasilisha Rasimu hiyo ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita John Paul Wanga amesema katika jumla kuu ya Tshs. 81,151,722,890 kiasi cha Tshs. 12,836,814,969 ni fedha za ruzuku zitakazotumika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo na Tshs. 3,003,960,860 ni ruzuku zitakazotumika kwa matumizi ya kawaida.
Rasimu hiyo imeendelea kufafanua kuwa kiasi cha Tshs.55,183.993,000 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi huku kiasi cha Tshs 4,486,875,000 ni makusanyo ya ndani ukiondoa mapato fungani.
Aidha Rasimu hiyo imebainisha kuwa kiasi cha Tshs. 2,692,125,600 ni matumizi ya kawaida ya mapato ya ndani na kiasi cha Tshs.1,794,750,400 ni mapato ya ndani kwa ajili ya shughuli za maendeleo huku kiasi cha Tshs. 510,844,000 ikiwa ni mapato mengine ambayo ni kama vile CHF, NHIF, DRF, Tozo za minara mashuleni na ada kwa kidato cha tano na sita.
Miongoni mwa vipaumbele vilivyozingatiwa katika Rasimu hiyo ni pamoja na kuboresha huduma za jamii kupitia sekta za Elimu, Afya, Ardhi, Mifugo na Uvuvi, Kilimo, na Maendeleo ya Jamii.
Wakati huo huo Halmashauri ya Wilaya ya Geita katika kuandaa na kutekeleza mpango na bajeti ya mwaka 2022/2023 imepanga kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile GGML, BUCKREEF, NELICO, PLAN INTERNATIONAL, MDH, KIVULINI, SONGAMBELE, ICAP, CODERT, na SEDIT.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe. Charles Kazungu ameshauri idara ya maendeleo ya jamii kutoa mikopo mikubwa kwa watu wachache ili iwe na tija zaidi, kuliko kugawanya kidogo kidogo kwa watu wengi suala linalochelewesha matokeo chanya huku akiwataka kutoa elimu kwa vikundi vyenye mikopo hiyo kurejesha kwa wakati ili na makundi mengine yanufaike.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa