Mkuu wa Idara: Daudi Lutema
Halmashauri ya wilaya ina eneo lenye jumla ya kiliometa za eneo 5,366.7. Eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 327,000. Eneo linalotumika kwa kilimo ni hekta 146,414.
Kilimo cha Umwagiliaji katika Wilaya kinafanyika kwa mazao mbalimbali kama Mpunga, Mbogamboga, Matunda, Mahindi na Maharage ya mabondeni.
Eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni Ha.13,160. Eneo linalolimwa kwa umwagiliaji ni Ha. 8,009, vyanzo vya maji ni Ziwa Victoria, Mito isiyokauka,chemchemi na maji ya mvua.
Uboreshaji wa miundombinu wa maeneo yanayofaa kwa kilimo utasaidia kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji na uzalishaji wa mazao kwa ujumla.
Idara ina jumla ya watumishi 33 ambapo walioko makao makuu ya Wilaya ni 7, walioko vijijini ni 24, walioko masomoni ni 1 na alieazimwa ni 1(Mkoani). Idara ina upungufu wa watumishi wa kilimo ambapo waliopo ni 33 na wanaohitajika ni 158 kufuatana na sera ya Taifa, kila kijiji katika wilaya kiwe na Afisa ugani.
Majukumu ya Msingi ya Idara;
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa